Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewataka viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuepuka kutoa kauli au kufanya vitendo vyenye taswira inayoweza kutafsiriwa kuwa baadhi yao wanashabikia ukandamizaji wa haki za wananchi.
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Nchimbi amesisitiza kuwa maneno na vitendo vya wana-CCM wakati wote lazima yaakisi dhamana ambayo chama kimepewa na wananchi ya kuwatumikia, ikiwemo kusimamia haki, bila ubaguzi wala dhuluma ya aina yoyote .
Balozi Nchimbi amesema hayo akiwa Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ihemi, mkoani Iringa, alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi za mikoa na wilaya zote, nchi nzima, leo Alhamis, 11 Julai 2024.
“Suala jingine ninataka kuwasisitiza UVCCM ni umuhimu wa watendaji wetu, viongozi wetu na wanachama wetu kutambua kuwa mnabeba taswira ya Chama chetu kila wakati, katika mnayosema au