You are currently viewing BIDHAA BANDIA ZA NGOZI KUTOKA NJE NI MWIBA KWA VIWANDA VYA NDANI..

BIDHAA BANDIA ZA NGOZI KUTOKA NJE NI MWIBA KWA VIWANDA VYA NDANI..

Na Gift Mongi
DAR ES SALAAM

Kwa kipindi kirefu sasa wazalishaji wa bidhaa za ngozi hapa nchini wamekuwa wakipita katika kipindi kigumu na ipo haja ya kuchukua jitihada za maksudi kunusuru hali hii.

Ugumu wa biashara hivi unatokana na kile kinachoelezwa ni uingizwaji holela wa bidhaa zenye mfanano na bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchni.

Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi (WOP)cha jiji Dr es Salaam Kenneth Woisso alisema ipo haja kwa sasa tume ya ushindani nchini FCC kuingilia kati ili kuokoa viwanda vya ndani.

‘Soko la bidhaa kutoka China ni kubwa na mbaya zaidi bidhaa zao ambazo sio ngozi halisi zinauzwa kwa bei ya chini hivyo sisi wazalishaji wa ndani tunapitia wakati mgumu’alisema Woisso

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo wa WOP aliiomba serikali kuona namna ya kuongeza tozo kwa bidhaa za ngozi zinazotoka nje ili kuwezesha kukua kwa viwanda vya ndani vya bidhaa hizo.

Alisema kuongeza tozo hiyo licha ya kupunguza uingizwaji wa bidhaa hizo kutaenda kuimarisha soko la ndani lakini pia kukua kwa mazao ya ngozi nchini

‘Tozo ikiwekwa nadhani wale wenye kuingiza hizi bidhaa watapungua hivyo viwanda vya ndani vitaenda kuongeza uzalishaji lakini mazao ya ngozi kwa ujumla yataenda kufanya vizuri’alisema

Kuna Kaskas ambaye ni mzalishaji mdogo wa bidhaa za ngozi alisema biashara hiyo kwa sasa inapitia wakati mgumu kutokana na soko kuingiliwa na bidhaa ambazo si halisi(bandia)za ngozi na kutaka jitihada za maksudi kufanyika ili kuokoa soko la ndani

‘Wenzetu China wana akili nyingi katika soko la hizi bidhaa utakuta zao ni nyingi na usipokuwa makini utadhani ni ngozi kumbe sio ni bandia sasa ifanyike hatua za maksudi ili tuponye viwanda vyetu’alisema

Leave a Reply