You are currently viewing MAMBO MANNE YA KIIMANI YANAYOFANANA KATIKA DINI YA UKRISTO NA UISLAMU.

MAMBO MANNE YA KIIMANI YANAYOFANANA KATIKA DINI YA UKRISTO NA UISLAMU.

Nexus

   ⛔Utangulizi.

Ukizungumzia dini kubwa za dunia basi moja kwa moja unazungumzia dini ya ukristo na dini ya uislamu… dini hizi ndio zenye wafuasi wengi zaidi duniani kuliko dini nyengine

Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zinasema kuwa dini ya ukristo ndio ina watu wengi zaidi ikiwa na watu zaidi ya billion 2.4 ambao ni sawa na asilimia 31 ya watu wanaoamini Mungu,

Uislamu ndio dini ya pili kwa kuwa na idadi ya watu wengi ikiwa na watu billion 1.9

Ukiachana na ukubwa huo wa wafuasi lakini pia dini hizi ukizifuatilia historia zake kwa undani zaidi basi utaangukia kwa watoto wa Ibrahim na ndio maana dini hizi mbili ukijumlisha na uyahudi basi huitwa dini za ibrahim (Ibrahimic Religions)

Ukiachana na muunganiko huo wa kihistoria, dini hizi mbili zina mambo mengi ya kiimani yanayofanana miongoni mwa mambo hayo ni kama yafuatayo;👇

✴1. MUNGU
Dini zote hizi za uislamu na ukristo zinaamini katika Mungu… Na wao wanaamini kuwa huyo Mungu ndie aliyeumba dunia na vilivyomo, Yeye ndie mwenye nguvu kuliko chochote wala lolote

Wanaamini kila jambo linatoka kwake liwe zuri au liwe baya ni Mungu ndio ameamua liwe maaana kama yeye asingeamua basi jambo hilo lisingekuwa

✴2. SIKU YA MWISHO
Dini zote hizi mbili zinaamini kuwa kuna siku ya mwisho ambayo watu wataekwa pamoja na kulipwa kila waliyokuwa wanayatenda duniani.

Utalipwa kulingana na matendo yako ulivyokuwa unayafanya duniani kama ulikuwa mtendaj mabaya basi utapewa adhabu na kama ulikuwa mtendaj wema utalipwa mazuri, na Dini zote hizi zinahamasisha waumini wake watende mambo mema.

✴3. SALA
Dini zote hizi mbili zinaamini kuwa sala/kusali ndio kitu kinachomuweka mtu kuwa karibu na Mungu. Usiposali basi huwa mbali na Mungu na ni rahisi kuingia kwenye maovu.

✴4. MAISHA BAADA YA KIFO
Dini zote mbili zinaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo, tofauti na baadhi ya dini nyengine zisizoamini kuwa kuna maisha baada ya kifo.

Uislamu na ukristo zinaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo na maisha hayo hutegemea matendo uliyokuwa unayafanya ukiwa hai, Kama ulikuwa mtu mtenda mena basi utaishi kwa amani na kama haukuwa mtenda mema basi maisha yako hayatokuwa na amani

Leave a Reply