You are currently viewing Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Afya, Malezi na Mazingira Baraza Kuu la Umoja wa WAZAZI CCM Taifa akabidhi tofari 1,000 ujenzi wa nyumba ya mtumishi

Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Afya, Malezi na Mazingira Baraza Kuu la Umoja wa WAZAZI CCM Taifa akabidhi tofari 1,000 ujenzi wa nyumba ya mtumishi

NA KIJA ELIAS, MWANGA.

Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Afya, Malezi na Mazingira ya Baraza Kuu la Umoja wa WAZAZI (CCM) Taifa, Bi. Catherine Ndamalya, amemkabidhi Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Mercry Marambo Mollel, tofari 1,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Bi. Catherine  Ndamalya amekabidhi tofari hizo Aprili 20, mwaka huu, baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba hiyo ambayo inajengwa eneo la  Kitongoji cha KIRURU-MTALANG’A Kata ya Mwanga, katika wiki ya maadhimisho ya Umoja.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Mercry Marambo Mollel,  amemshukuru mdau huyo wa maendeleo  kwa kuweza kuchangia ujenzi wa nyumba hiyo ya mtumishi.

“Makatibu ndio watendaji wakuu ambao wanaratibu shughuli zote za Jumuiya ya Wazazi,  lakini wamekuwa wakiishi kwenye nyumba za kupanga  mtaani, hali ambalo wamekuwa kikumbana na changamoto mbalimbali na hivyo kushinda kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa.wa Kilimanjaro Chifu Daudi Babu Mrindoko, amesema ujenzi wa nyumba za watumishi ni kuwapunguzia gharama za wao kwenda kuoshi katika nyumba ,a kupanga.

“Tuanataka mtumishi wa Jumuiya ya WAZAZI  anapoletwa kikazi ndani ya mkoa wa Kilimanjaro, aweze kukuta nyumba ya kuishi hatutaki tena mtumishi aende kuishi kwenye nyumba ya kupanga, tayari nyumba kama hii tumesha jenga Siha, Rombo na sasa wilaya ya Mwanga,”amesema Chifu Mrindoko.

Maadhimisho  ya Wiki ya Jumuiya ya WAZAZI Mkoa wa Kilimanjaro, yamefanyika kimkoa  katika Shule ya Sekondari Mwanga inayomilikiwa na Jumuiya  na kuhudhuriwa na Viongozi wa Chama na Jumuiya zake.

MWISHO.

This Post Has One Comment

Leave a Reply