DODOMA: Mwanafunzi wa Kiume wa Mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye Jina lake halijawekwa wazi, inadaiwa amefanya jaribio la kutaka kujiua alipokuwa Ghorofa ya Nne ya (Block H, College of Education) Chuoni hapo, ikidaiwa ni baada ya kutokea mgogoro wa kimapenzi na mwenza wake ambaye bado hajafahamika
KOMKYA NEXUS imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami kuhusu taarifa hizo ambapo amesema “Taarifa hizo ni za kweli, huyo Kijana alitaka kujiua, bado sijafahamu njia aliyotumia kutaka kutimiza lengo lake hilo lakini ameumia na amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa akiendelea na matibabu.”
Ameongeza “Taarifa za awali zinaonesha chanzo ni masuala ya mapenzi. Uongozi wa chuo umekabidhi suala hilo kwa Mamlaka za Usalama huku tukisubiri apate nafuu kisha mchakato mwingine ufuate ikiwemo kupatiwa ushauri wa Kisaikolojia.”