You are currently viewing SERIKALI IMETUTENDEA HAKI WAZALISHAJI WA NDANI BIDHAA ZA NGOZI.

SERIKALI IMETUTENDEA HAKI WAZALISHAJI WA NDANI BIDHAA ZA NGOZI.

Na Gift Mongi
Dar es Salaam

Kwa siku za usoni wazalishaji wa ndani wa bidhaa za ngozi walikuwa wakikabiliwa na uingizwaji wa bidhaa bandia za ngozi kutoka nje jambo lililohatarisha uhai wa viwanda vya ndani.

Ugumu wa biashara hii unatokana na kile kinachoelezwa ni uingizwaji holela wa bidhaa zenye mfanano na bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchni.
Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi (WOP)cha jiji Dr es Salaam Kenneth Woisso alisema ipo haja kwa sasa tume ya ushindani nchini FCC kuingilia kati ili kuokoa viwanda vya ndani.

‘Soko la bidhaa kutoka China ni kubwa na mbaya zaidi bidhaa zao ambazo sio ngozi halisi zinauzwa kwa bei ya chini hivyo sisi wazalishaji wa ndani tunapitia wakati mgumu’alisema Woisso

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo wa WOP aliiomba serikali kuona namna ya kuongeza tozo kwa bidhaa za ngozi zinazotoka nje ili kuwezesha kukua kwa viwanda vya ndani vya bidhaa hizo.

Alisema kuongeza tozo hiyo licha ya kupunguza uingizwaji wa bidhaa hizo kutaenda kuimarisha soko la ndani lakini pia kukua kwa mazao ya ngozi nchini

‘Tozo ikiwekwa nadhani wale wenye kuingiza hizi bidhaa watapungua hivyo viwanda vya ndani vitaenda kuongeza uzalishaji lakini mazao ya ngozi kwa ujumla yataenda kufanya vizuri’alisema

Katika kuonyesha kuwa serikali imesikia kilio hicho cha wazalishaji wa ndani bidhaa za ngozi katika bajeti iliyosomwa hivi karibuni bidhaa hizo kutoka nje zitaongezwa tozo ili kuhakikisha wazalishaji wazawa wanafanya vizuri

Kuongezwa kwa tozo hiyo ni hatua mojawapo katika kupunguza bidhaa bandia za ngozi na mazao yake ambavyo vyote vinapatikana hapa nchni.

Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba akisoma bajeti hiyo ya mwaka 2024/2025 alisema katika kuhakikisha wazalishaji wazawa wanafanya vizuri ndio sababu ya kuongeza tozo hiyo.

Mwisho.

Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba akisoma bajeti hiyo ya mwaka 2024/2025 alisema katika kuhakikisha wazalishaji wazawa wanafanya vizuri ndio sababu ya kuongeza tozo hiyo.

Mwisho.

Leave a Reply