You are currently viewing SOKO LA NDANI BIDHAA ZA NGOZI KUIMARIKA ZAIDI NI BAADA YA SERIKALI KUSIKIA KILIO CHA WAZALISHAJI HAO

SOKO LA NDANI BIDHAA ZA NGOZI KUIMARIKA ZAIDI NI BAADA YA SERIKALI KUSIKIA KILIO CHA WAZALISHAJI HAO

Na Gift Mongi
Dar es Salaam

Baada ya kilio cha muda mrefu cha wazalishaji wa bidhaa za ngozi juu ya soko kuvamiwa na bidhaa bandia sasa mwarobaini umepatikana.

Kupatikana kwa mwarobaini huo kunaenda kuleta matumaini makubwa kwa wazalishaji wa bidhaa hizo hususan kwa wale wa ndani ya nchi

Mwarobaini ambao wazalishaji hao walikuwa wakiupendekeza mara kwa mara ni pamoja na kuongeza tozo kwa bidhaa za ngozi zinazoingizwa kutoka nje lengo likiwa ni kukuza soko la ndani la bidhaa hizo.

Kenneth Woisso ni mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza bidhaa hizo kijulikanacho kama (WOP)yaani Woisso Original Products ambapo alisema kubwa changamoto haikuwa uingizwaji tu bali hata bei sokoni ilikuwa chini.

“Tatizo sio kuingiza tu bidhaa hizo kwanza hazina ubora maana sio ngozi halisi lakini pia ziliuzwa kwa bei ya chini ikilinganishwa na hizi za kwetu”alisema

Alisema sasa mara baada ya serikali kuongeza tozo na ushuru kwa bidhaa za ngozi kutoka nje ni dhahiri kuwa sekta hiyo itaenda kufanya vizuri msanii hali ilishaanza kubwa ni mbaya.

“Hata kama wataingoza haitaweza kufikia kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa kama mafuriko lakini kutokana na tozo zenyewe hawawezi kuuza kwa bei ya chini tena’alisema

Kwa kujibu wa Woisso ni kuwa wateja walio wengi hupenda vitu vya bei rahisi kutokana na hali ya kipato ilivyo hivyo bidhaa ambazo zina mfanano na ngozi wengi hukimbilia jambo ambalo kwao ni hasara.

“Kama ukinunua kiatu cha ngozi halisi unaweza kudumu nacho hata miaka 5 ila ngozi bandia mwaka mmoja haumaliziki na utofauti katika bei utakuta ni elfu 5000 tu HII ni kama kuukaribisha umaskini

Soko la bidhaa kutoka China ni kubwa na mbaya zaidi bidhaa zao ambazo sio ngozi halisi zinauzwa kwa bei ya chini hivyo sisi wazalishaji wa ndani tunapitia wakati mgumu’alisema Woisso

Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba akisoma bajeti hiyo ya mwaka 2024/2025 alisema katika kuhakikisha wazalishaji wazawa wanafanya vizuri ndio sababu ya kuongeza tozo hiyo.

Mwisho.

Leave a Reply