You are currently viewing MJUE SHUJAA SHEKILANGO MWENYEWE MWENYE JINA LA BARABARA YA SHEKILANGO, NA NAMNA ALIVYOPOTEZA MAISHA

MJUE SHUJAA SHEKILANGO MWENYEWE MWENYE JINA LA BARABARA YA SHEKILANGO, NA NAMNA ALIVYOPOTEZA MAISHA

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama ‘Shekilango Road’, ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng’oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling’olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji.

Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe.

Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

This Post Has One Comment

Leave a Reply