Vingozi mbalimbali wa CCM wameaswa kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura katikati mwa mwezi julai ili ifikapo wakati wa Uchaguzi waweze kuwachagua Vingozi wanao wataka.
Hayo yamezungumzwa leo na Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini alipofika kutoa Semina kwa vingozi hao.
” ili kupata viongozi bora basi twendeni tukahamasishe wananchi waende kujiandikisha muda ukifika watimize haki yao ya Msingi ya kupiga kura” alisema Mahanyu
Pia Mahanyu amewaeleza vingozi hao kwamba hakuna chama cha upinzani ambacho kinaweza kuleta maendeleo ya Kweli katika jamii ambapo alizungumza akiwa kata ya Mabogini, akirejea picha ya miaka ya nyuma 2014 na 2015 ambapo CCM ilipoteza baadhi ya Vitongoji, Vijiji, Kata na Majimbo wananchi wakachagua upinzani hivyo kupelekea Maendeleo yakadorola kwasababu Viongozi walikuwa hawaeni kwasababu wapinzani kazi yao ni kupinga na wakati mwingine walikuwa wakitoka bungeni wakati wa kujadili hoja za maendeleo katika majimbo yao.
” Vingozi hakuna Mpinzani anaeweza kuleta Maendeleo ya kweli katika Jamii yetu isipokuwa Mama Samia Suluhu Hassan na CCM ” alisema Mahanyu
Hayo aliyasema alipofanya ziara yake na mafunzo na Seckretarieti yake katika Kata ya Mabogini na Arusha Chini ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya CCM Wilaya ya Moshi Vijijini