MBUNGE ATAKA UPENDELEO KWA WAWEKEZAJI WAZAWA.

Na Gift Mongi
Dodoma

Uwekezaji huleta fursa!ndio tena kwa wazawa na wasio wazawa lakini pia maendeleo katika jamii inayoizunguka.

Mfano tumeshuhudia wawekezaji wengi wakirudisha faida waliyoipata kwa jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya maji miundombinu na vinginevyo vingi tu!

Lakini katika kuhakikisha haya yote yanaenda hatuna budi kuweka mazingira rafiki katika kuvutia uwekezaji huu ambao unaonekana kuwa sehemu ya chuchu katika uchumi wetu.

Tutakubaliana kuwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan anayeongoza serikali ya awamu ya sita amekuwa kinara katika kupambana kupata wawekezaji kwenye miradi mbalimbali

Katika kuhakikisha dira na dhamira ya rais Dkt Samia inatimia ni lazima jitihada ziwepo katika kila nyanja ikiwemo mtu mmoja mmoja au katika ngazi za uwakilishi.

Katika mantiki hiyo mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini(CCM) Profesa Patrick Ndakidemi aliuliza swali la papo kwa hapo kwa waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kama ifuatavyo:

KWENYE MIPANGO YA KUBORESHA UCHUMI NA KULIONGEZEA KIPATO TAIFA LETU, SERIKALI IMEREKEBISHA SERA ZAKE KATIKA MAENEO MBALIMBALI ILI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI WA NDANI NA WA NJE. SEKTA AMBAZO ZIMEVUTIA WAWEKEZAJI WENGI NI ZA VIWANDA, BIASHARA, MADINI, KILIMO NA UTALII.

JE? SERIKALI INA MIKAKATI GANI YA KISERA YA KUWAPENDELEA WAWEKEZAJI WAZAWA ILI WAWEZE KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUSAIDIA KUKUZA UCHUMI ENDELEVU WA TAIFA LETU?

Swali hilo liliweza kujibiwa na waziri mkuu kama anavyofanya hapa..

Leave a Reply