You are currently viewing MWENYEKITI CCM MOSHI VIJIJINI ASISITIZA USHINDI WA UCHAGUZI NI NAMBA

MWENYEKITI CCM MOSHI VIJIJINI ASISITIZA USHINDI WA UCHAGUZI NI NAMBA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi vijijini Ndugu Siril Mushi amesisitiza ili chama chetu kiweze kushinda uchaguzi kinategemea wingi wa namba inayotegemea idadi ya wanachama wake kama mtaji, umoja ndani ya chama na miongoni mwa wanachama, rekodi ya utendaji kazi pamoja na kuweka wagombea waadilifu na wanaokubalika na jamii.

Ndugu Siril ameeleza hayo katika ziara yake aliyoifanya katika kata ya Makuyuni Jimbo la Vunjo alipokuwa akizungumza na wanaCCM kwenye mkutano wa ndani.

Katika hatua nyingine amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kukiamini chama hicho katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa 2024 kama shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 – 2025.

Katika hatua nyingine Katibu wa CCM wilaya ya
Moshi Vijijini Ndugu Ramadhan Mahanyu amewataka wanaCCM kutangaza kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ili wananchi wafahamu kazi nzuri inayofanywa na serikali ya CCM Awamu ya 6 chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katika kufanikisha uwekaji wa kumbukumbu za wanachama Ndugu Siril amekabidhi vitabu 30 kwa ajili ya mabalozi kata ya Makuyuni vilivyotolewa na Mbunge Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei.

Ziara hii ya uhamasishaji wa serikali za mitaa, uimarishaji chama na usikilizaji wa kero za wananchi inaendelea kesho katika kata za Kirua Vunjo Kusini na Kahe Mashariki. Katika ziara hii walikuwepo pia Bi. Esther Kway mjumbe wa kamati ya siasa wilaya na Shakila Singano katibu wa UWT Wilaya.

Leave a Reply