Na Gift Mongi
Moshi
Vijana wana jambo lao!ndio huwezi weweseka wakifanya yao na ndio maana wanasema vijana ni jeshi kubwa katika ujenzi wa nchi na chama (CCM).
Kadhalika vijana wanatambulika kama maono ya taifa kwa siku zijazo na ndio maana baadhi wanaaminika na kupewa nafasi nyeti serikalini.
Kwa muktadha huu bado naamini vijana ni chache ya uongozi katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi yetu pendwa yaani TANZANIA.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuven Shirima ni miongoni mwa vijana waliojitokeza wazi katika kuijenga Moshi lakini pia chama kwa ujumla
Katika kuonesha ‘umwamba’ huo ameshiriki bonanza la mpira wa miguu katika kata ya Makuyuni mwenyekiti Yuvenali Shirima amedhamini mipira saba 7 yenye thamani ya Tsh 525000 :
Je ni jambo gani la kujivunia?hapa anaonesha chachu ya vijana kunielewa na kuwa msaada kwa wengine badala ya kuwa mzigo maanisha mzigo kwenye familia.
Cde Shirima bado jambo lako ni endelevu tuje huku chini kabisa tuna vijana wengi tu ambao ndio msingi wa chama
Mwisho