You are currently viewing Biden atetea kumwita Trump tishio kwa demokrasia
President Joe Biden poses for his official portrait Wednesday, March 3, 2021, in the Library of the White House. (Official White House Photo by Adam Schultz)

Biden atetea kumwita Trump tishio kwa demokrasia

Official portrait of President Donald J. Trump, Friday, October 6, 2017. (Official White House photo by Shealah Craighead)

Rais wa Marekani Joe Biden ametetea matamshi yake dhidi ya Donald Trump na kusema kwa nini ilikuwa muhimu, katika mahojiano yake ya kwanza tangu jaribio la mauaji ya mpinzani wake wa kisiasa.

Rais alisema kampeni yake ilikuwa na jukumu la kuwasilisha kwa uwazi tishio la muhula wa pili wa Trump, na kuongeza kuwa maneno yake sio yale yanayohitaji kupunguzwa makali.

Hata hivyo, alimwambia Lester Holt wa NBC kwamba lilikuwa “kosa” kusema ulikuwa “wakati wa kumwangazia Trump” wakati wa kukutana na wafadhili siku chache kabla ya jaribio la kumuua Trump lililotokea katika mkutano wa Jumamosi huko Pennsylvania.

Bw Biden alisema anamaanisha kuwa Wanademokrat wanapaswa kuzingatia zaidi Trump, sera zake na taarifa za uongo alizotoa wakati wa mjadala wa urais mwishoni mwa mwezi uliopita.

Wakati wote wa mahojiano, Bw Biden aliweka wazi kuwa hatajiondoa katika kinyang’anyiro cha urais – licha ya wito kutoka kwa wanachama wa chama chake baada ya utendakazi wake duni kwenye mjadala.

“Mimi ni mzee,” alisema, huku pia akibainisha kuwa yeye na Trump wamepishana kwa miaka mitatu pekee. Alisema uwezo wake wa kiakili ulikuwa mzuri na aliorodhesha mafanikio yake kama rais – lakini alikubali kwamba alikuwa akifanya kazi ili kuwahakikishia Wamarekani yuko sawa kushika nafasi hiyo.

“Ninaelewa kwa nini watu husema, ‘Mungu wangu, ana umri wa miaka 81. Lo. Atakuwa vipi atakapokuwa na umri wa miaka 83, miaka 84?’ Ni swali zuri kujiuliza,” alisema.

Aliongeza kuwa imani yake iko kwa wapiga kura ambao kwa kiasi kikubwa walimuunga mkono katika mchujo wa chama cha Democratic. “Nawasikiliza.”.

Trump aliyefungwa bandeji akaribishwa kwa nderemo katika kongamano la chama cha Republican

Rais Donald Trump amehudhuria mkutano wa chama cha Republican akikaribishwa kwa shangwe na nderemo.

Hii ni mara ya kwanza kwake kuonekana kwenye hafla kubwa ya umma tangu jaribio la mauaji dhidi yake kwenye mkutano wa kisiasa siku ya Jumamosi.

Bandeji iliyokuwa kwenye sikio la Trump ilionekana wazi huku akichukua nafasi yake karibu na mgombea mwenza wake, JD Vance.

Wafuasi wa Republican walikuwa na furaha isiyokifani.

Walianza kuimba “U-S-A, U-S-A” na kuendelea kusema “Pambana! Pambana! Pambana!” huku wakirusha ngumi hewani, ishara kwamba wengi hapa wamemkubali baada ya Trump kuonyesha kuwa imara alipokuwa anashuka jukwaani baada ya kupigwa risasi huko Pennsylvania.

Wengine waliokuwepo ni pamoja na wanafamilia, kama vile wanawe Eric na Donald Jr.

Rais huyo wa zamani alionekana kutabasamu na kupiga makofi wakati wote wa hotuba.

Mara kwa mara aliwageukiwa Vance na Donald kutoa maoni juu ya kile kilichosikika

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

Leave a Reply