“Mheshimiwa mgeni rasmi (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo) mpaka sasa Arusha iko shwari na kesho tarehe 01.05.2024 (Mei mosi Day) tutatangaza kwamba katika mji salama Tanzania namba moja ni Arusha, kwa hiyo wananchi wote wa Tanzania na wageni wote ni vyema wajuwe kuwa wakitaka kwenda kwenye jiji ambalo ni salama na lenye hali ya hewa ambayo ni nzuri katika nchi hii wawawe kuja Arusha, tuna kila sababu ya kuwa na kila aina ya mgeni kwa sababu mazingira sasa yanazidi kuboreshwa chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan” -Makonda
“Napenda kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukupa nafasi wewe (Prof. Kitila Mkumbo) kuwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji, unastahili nafasi hiyo kwa sababu wewe ni brain kati ya brain tulizonazo katika nchi yetu ya Tanzania si tu kwa sababu ya taaluma yako lakini pia uthubutu wako wa kutazama mambo nje ya box, na kuona namna gani tunaweza kusukuma gurudumu na kufikia hatua ya kuleta mafanikio kwa watu wote” -Makonda
“Nakumbuka tarehe 18.04.2024 tulipokutana Dodoma kwenye siku ya kuzindua mpango wa Dira na ukusanyaji wa maoni tulipata nafasi ya kuteta nawe pamoja na Katibu Mkuu (Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji) na tukakubaliana kwamba lazima tuanze, pamoja na changamoto na maandalizi ya Mei mosi lakini ukasema lazima tuanze, na sasa huu ni mwanzo nzuri kuwapata watu takribani 400 wanakuja kwenye ukumbi na kuja kusikiliza maelekezo, mawazo kuelekea kwenye kuimarisha uwekezaji katika mkoa wetu, hii ni dalili njema naomba nikupongeze na kukushukuru sana” -Makonda
Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Arusha amezungumza hayo leo, Jumanne Aprili 30.2024 alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji wa sekta ya utalii lililofanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha