You are currently viewing DUNIA INATAMBUA MCHANGO WA RAIS DKT SAMIA…PROF NDAKIDEMI

DUNIA INATAMBUA MCHANGO WA RAIS DKT SAMIA…PROF NDAKIDEMI

Na Gift Mongi
Moshi.

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani machi 2021 amepewa tuzo za udaktari wa heshima katika vyuo vitano tofauti tofauti ndani na nje ya nchi.

Udaktari huu wa heshima ambao amekuwa akipewa rais kumetajwa kubwa ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya ambayo inaonekana duniani kote.

Mbunge wa jimbo la Vunjo Prof Patrick Ndakidemi anasema kuwa dunia imetambua juhudi za Rais wetu katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu na kuboresha mahusiano na mataifa rafiki.

Ametambulika kutokana na mabadiliko makubwa ya maendeleo aliyoyaleta kwenye sekta mbalimbali tangu alipoingia madarakani Machi 2021.

‘Ameweza kujipambanua katika nyanja mbali mbali na hakuna asiyeyaona haya mazuri ambayo yanafanyika au yameshafanyika kwa kipindi ambacho amekuwa rais’Anasema

Aliongeza kutambulika kwake kunatuongezea heshima ya kimataifa na kuboresha diplomasia yetu ya uchumi wa kimataifa.

Naye mkazi wa Kibosho Kirima Onesmo Mushi alisema rais Dkt Samia Suluhu Hassan anastahili tuzo hizi za udaktari wa heshima kwa namna ambavyo ameifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Alisema kwa sasa dunia inaijua Tanzania lakini hata sisi hapa nchini tumeshuhudia mambo mengi na makubwa yakifanyika hivyo heshima ya udaktari kwake sio bahati mbaya na anastahili.

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

Leave a Reply