You are currently viewing MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI ASHIRIKI ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI ASHIRIKI ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA

Na Gift Mongi

Moshi

Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi leo t ameungana na mamia ya wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini na jimbo la Vunjo katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr. Emanuel Nchimbi, pamoja na Katibu Itikadi na Uenezi Na Mafunzo CCM taifa Comrade Amos Gabriel Makala, Katibu wa NEC Organaizesheni ndugu Issa Gavu, na Rabia Abdallah Hamid Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa Kimataifa.

Akizungumza katika eneo la Njia Panda,Prof Ndakidemi alieleza kuwa hadi kufikia Desemba 2023 jimbo la Moshi Vijijini lilishapata miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 42.

Alimshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa miradi iliyokuja katika Kata zote 16 za Jimbo la Moshi vijijini.

Aidha alimueleza katibu Mkuu kuwa changamoto kubwa inayoikabili Jimbo lake ni ubovu wa barabara.

Alisema, barabara hizo hazitengenezwi kwa wakati zikiwemo zile zilizoko katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na ahadi mbalimbali za viongozi.

Amemwomba Katibu Mkuu kuhimiza utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya CCM na ahadi za viongozi wakuu.

Aliomba kwa kuwa TARURA na TANROADS wana mambo mengi, basi fedha inayotolewa na TANAPA kwa maendeleo ya jamii (Corporate Social Responsibility) itumike kuzijenga barabara zilizoko katika vijiji vyote vinavyopakana na mlima Kilimanjaro katika wilaya za Siha, Hai, Moshi na Rombo

Mwisho

Leave a Reply