đź“ŤAlbert Einstein aliulizwa swali kuwa akili ni nini?
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya “digrii” walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.
Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.
Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.
Akili siku zote ni “superior” kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?
So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.
Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, WhatsApp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona “kilaza” darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na “kilaza” mwenye Akili.
Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.
Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?
Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa “AKILI”. Na kama hamna kinachobakia basi hicho kichwa hakina tofauti na mtungi wa gesi ambao umetumika na gesi kwisha.
Asante kwa kusoma.