You are currently viewing Mbunge wa Afrika Mashariki Dunia

Mbunge wa Afrika Mashariki Dunia

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kusaidia wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi ya FUNGUA TRUST, Dk. Shogo Richard Mlozi amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za kifo hicho zimetangazwa leo Alhamisi bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson kabla ya kuanza kwa kikao cha 47 cha Mkutano wa Bunge la Bajeti.

“Leo asubuhi tumepokea taarifa kwamba Mheshimiwa Dk. Shogo Richard Mlozi ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatunaye tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za ziada tutawataarifu, tusimame kwa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho,” amesema Dk. Tulia

Dk. Mlozi ambaye alichaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika bunge hilo mwaka 2022, alikuwa anahudumu katika nafasi hiyo hadi 2027.

Leave a Reply