KUWAKUTANISHA WANANDOA LENGO NI KUNUSURU HALI ILIYOPO ISIONGEZEKE ZAIDI
Na Gift Mongi
MOSHI
ASKOFU mstaafu wa kanisa la Tanzania assemblies of God (TAG)jimbo la Kilimanjaro Magharibi Dkt Glorious Shoo amekemea vikali tabia ya mienendo vya vitendo vinavyopotosha na kuharibu jamii na kutaka kila anayechukizwa kukemea.
Amesema matendo yanayotokea hivi sasa ikiwemo suala la mapenzi ya jinsia moja na ulawiti sio mambo ambayo yanatakiwa kunyamaziwa bali kutumia nguvu kubwa katika kuyakataa.
‘Nawakutanisha wanandoa na wale wasio wanandoa lengo likiwa ni kuwakumbusha wajibu wao na kuhusu mambo ambayo yanaendelea kwa kasi ambayo jamii zetu ndio waathirika wakuu na kuwa tunatakiwa kuipinga jamii kabla mambo hayajawa mabaya zaidi’anasema
Mwisho.