You are currently viewing Moshi DC kujipanga kuanza Biashara ya Hewa Ukaa ~

Moshi DC kujipanga kuanza Biashara ya Hewa Ukaa ~

Ziara ya Ujerumani ya Mwenyekiti wa Halmashauri imeleta Manufaa ya biashara ya hewa ukaa.

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ya jipanga kuanza biashara ya hewa ukaa

Lengo ni kuhakikisha wananchi wa Moshi Vijijini wanafaidika kiuchumi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda miti.

Hayo yamebainika leo kati ya kikao na mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Morris Makoi na viongozi wanaomiliki Mashamba ya vyama vya msingi na Madiwani wanaoishi katika maeneo hayo akiwepo Mhe. Bahati Mamboma Diwani kata ya Kibosho kato, Mhe. Adv. Wilhad Kitali Diwani kata ya Uru Kusini, Mhe. Samweli Materu Diwani kata ya Uru Mashariki, Christopher Ndakidemi Diwani kata Kibosho Mashariki na Samweli Kirumbuyo Diwani kata ya Kibosho Kindi alipokutana nao katika kikao maalumu cha mrejesho wa ziara yake Nchini Ujerumani ambapo Madiwani wa Kata husika nao walialikwa kuhudhuria

Wananchi wata hamasishwa kupanda miti kama sehemu ya kutunza mazingira lakini pia wata nufaika kiuchumi kwa kuuza hewa safi itakayo tokana na miti.

Walikuwepo wawezeshaji kutoka kampuni ya Carbon Sink International Company Limited ambapo walielezea umuhimu wa hewa Ukaa na namna wananchi pamoja na Halmashauri inavyoweza kunufaika.

Aidha morris Makoi ametoa mifano mingi waliyoikuta kutoka Ujerumani hewa Ukaa imekuwa ikiwabeba Halmashauri nyingi hususani Ujerumani kwa kurudisha faida kwenye jamii na Wananchi

” Katika Halmashauri zilizoendelea zimeweza kujenga Ofisi za Vijiji kuwezesha Vikundi mbalimbali vya Wajasiliamali na mwananchi Mmoja mmoja pamoja na kujenga shule na zahanati” Mhe. Makoi

” Ipo mifano ya baadhi ya Halmashauri zilizo nufaika sana na biashara hii ya hewa ukaa hapa Tanzania kama vile Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika iliyopo katika Mkoa wa Katavi,

Pia Wilaya ya pangani wameanza mikakati ya kuanza biashara hii ya hewa Ukaa”

Leave a Reply