You are currently viewing Chama cha ANC kimewasiliana na vyama vinavyotaka kuunda serikali mpya

Chama cha ANC kimewasiliana na vyama vinavyotaka kuunda serikali mpya

Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini kinasema kuwa imezifikia pande zote ambazo zina nia ya kuchangia kuunda serikali mpya.

Katika kikao na wanahabari msemaji Mahlengi Bhengu-Motsiri alisema kwa wakati huu ANC inaegemea upande wa serikali ya umoja wa kitaifa, akidai kuwa wapiga kura wanataka vyama vyote kufanya kazi pamoja kwa sababu hakuna aliyepata wingi wa kura.

Chama cha ANC kilipoteza idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi wa wiki iliyopita kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, lakini bado ndicho chama kikubwa zaidi na kinaongoza katika kuunda serikali mpya.

Bi.Bhengu Motsiri alisema ANC ilikuwa inazungumza na chama cha Democratic Alliance, chama cha Marxist Ecomic Freedom Fighters, pamoja na vyama vingine vidogo.

Alisema chama cha kwanza cha MK cha rais wa zamani Jacob Zuma, ambacho kilipata nafasi ya tatu kwa asilimia 15 ya kura, hakijajibu, lakini mlango wa ANC ulibaki wazi. Uamuzi wa mwisho unafanywa na kamati kuu ya kitaifa, ambayo itakutana Alhamisi.

Leave a Reply