You are currently viewing RAS Kilimanjaro afariki dunia kwa ajali

RAS Kilimanjaro afariki dunia kwa ajali

Hai.Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki dunia katika ajali ambayo imetokea eneo la Njia panda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa kwenye ziara Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kwamba ajali hiyo imetokea muda wa saa 8 kuelekea saa 9 mchana leo, Juni 18, 2024.

“Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,”amesema RC Babu

Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Katika ajali hiyo inadaiwa kuwa, dereva wake naye kafariki duniani.

Mwisho

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

Leave a Reply