You are currently viewing HALMASHAURI ZENYE UHABA WA WALIMU KUPEWA KIPAUMBELE KWENYE AJIRA MPYA ​

HALMASHAURI ZENYE UHABA WA WALIMU KUPEWA KIPAUMBELE KWENYE AJIRA MPYA ​

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu), Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amesema Ajira mpya za Kada ya Ualimu zitakazotolewa hivi karibuni mgawanyo wa walimu utazingatia Halmashauri zenye uhaba wa walimu.

Mhe. Katimba ameyasema katika mkutano wa 15 kikao cha 52 cha Bunge la Bajeti linaloendelea jijini Dodoma leo tarehe 24.06.2024 kwa mwaka 2024/25 Serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 Shule za Msingi na Sekondari watapangiwa vituo vya kazi hususani Halmashauri zenye upungufu.

Mhe. Katimba amesisitiza Halmashauri kufanya msawazo wa walimu kwa kupunguza walimu mjini na kuwapeleka vijijini ili kupunguza ukali wa upungufu wa walimu katika maeneo ya vijiji huku Serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga nyumba.

This Post Has One Comment

  1. Клининговая компания: прайс лист и цены на уборку
    клининг стоимость за 1 кв м [url=genuborkachistota.ru]genuborkachistota.ru[/url] .

Leave a Reply