You are currently viewing Historia imeandikwa Mwanga – Kilimanjaro Ziara ya Katibu Mkuu CCM

Historia imeandikwa Mwanga – Kilimanjaro Ziara ya Katibu Mkuu CCM

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Rabia Hamid Abdallah akifafanua Jambo mbele ya wananchi wa Mwanga Kilimanjaro Waliohudhuria kumsikiliza Katibu Mkuu, Dk. Emmanuel Nchimbi
~Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Gavu akizungumza na wananchi waliojitokeza

Melfu ya Wananchi wa Wilaya ya Mwaka Mkoani Kilimanjaro wamejitokeza kwa wingi kumpokea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi pamoja na Msafara wake leo Juni 06, 2024 ambapo kiongozi huyo amewahutubia mambo mbalimbali ikiwemo suala la kudumisha amani na baadae kusikiliza Kero mbalimbali za Wananchi wa eneo hilo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Mji wa Mwanga katika Uwanja wa CD Msuya, uliopo mjini Mwanga, Alhamis Juni 6, 2024, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Dkt Nchimbi ameongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Rabia Hamid Abdallah pamoja na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Gavu.

Leave a Reply