#KOMKYA NEXUS. Kufuatia utendaji Mzuri wa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan baadhi ya vigogo wa vyama vya upinzani wamejitokeza kwa Wingi na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Aliyekuwa kuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya hatimae Kuwa Katibu wa Wilaya Chadema Ndg. Kharifa Mndeme amejiunga na CCM na kuelezea kuvutiwa na utendaji kazi wa Chama hicho ambacho kinafuata misingi ya Demokrasia na Utawala bora,
Hayo yamejili wakati Ziara ya Sekretarieti ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mwenyekiti wake Bi. Mercy Mollel Wilaya ya Mwanga alipotembelea Tarafa ya Usangi kwa ziara ya Kikazi.