You are currently viewing MAENDELEO YALIYOLETWA MANISPAA NI UPENDELEO

MAENDELEO YALIYOLETWA MANISPAA NI UPENDELEO

#KOMKYA NEXUS. Mbunge wa jimbo la Moshi Priscus Tarimo mapema leo ameeleza maendeleo yaliyokuja Jimbo la Moshi ni upendeleo ambao wananchi waliamua kukichagua chama cha Mapinduzi

Katika kipindi cha Miaka minne miongoni mwa ahadi alizo ahidi 10 zimetekelezwa ahadi 9 isipokuwa 1 pekee huku akijipambanua kwa kuwaletea maendeleo makubwa Manispaa ya Moshi.

Tarimo amefanikiwa kuleta hospitali ya wilaya zaidi ya Bil. 7.5 zimetolewa kuhakikisha inajengwa ya kisasa na nipekee ya ghorofa.

Aidha gari za ambulesi 3 zimeletwa manispaa na gari moja la zimamoto, hoja binafsi zilitolewa na mbunge huyo na imepita bila kupingwa kwa asilimia zote.

Hayo ni baadhi ya mambo mengi na makubwa yamliyoletwa na serikali ya CCM, hivyo amewataka wana CCM na wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa CCM inashinda kwa kishindo.

Leave a Reply