Makonda atinga Makao Makuu ya CCM Dodoma kuhojiwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.
Makonda ameitikia wito wa kufika mbele ya kamati hiyo kwa barua aliyoandikiwa Aprili 16, 2024 huku sababu za kuitwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi.
Awali, Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 kabla ya kusogezwa mbele na kupangwa kufanyika leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.
Komkya Nexus inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kwenye ofisi hizo