You are currently viewing MBUNGE ATAKA KUJUA LINI KATA YA KIMOCHI ITAKUWA NA UPATIKANAJI WA MAJI WA KUTOSHA?

MBUNGE ATAKA KUJUA LINI KATA YA KIMOCHI ITAKUWA NA UPATIKANAJI WA MAJI WA KUTOSHA?

Na Gift Mongi
Dodoma

Shida ya maji katika baadhi ya maeneo ya vijijini bado inaonekana kubwa ni tatizo linalochangia kukwamisha shughuli nyingi za kimaendeleo.

HII maana yake ni kuwa badala ya kufanya shughuli za uzalishaji maji na kujiingizia kipato muda mwingi hutumika katika kutafuta maji.

Itakumbukwa kuwa katika shughuli hiyo ya utafutaji maji wanaoonekana kubeba jukumu hili katika familia ni wanawake kwa nafasi kubwa ikilinganishwa na idadi ya wanaume.

Hapa ndipo serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ilivyokuja na mpango wa kumtua mama ndoo kichwani lengo ni kuondoa adha hiyo ya kipindi kirefu.

Katika majimbo ya vijijini bado kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa maji bado ni wakusuasua na hapa ndipo utakapowasikia waheshimiwa wabunge wakielekeza kilio chao kwa serikali kutaka kujua hatima ya wapiga kura wao.

Mfano leo june 12.2024 bungeni jijini Dododoma mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi aliuliza swali la nyongeza bungeni ambapo alihoji mpango wa Serikali kupeleka maji katika vijiji vya Mdawi, Sango, Shia na Kisaseni katika Kata ya Kimochi ?

Hata hivyo swali hilo liliweza kujibiwa na serikali kutoka kwa Mhe. Eng. Kundo Andrea Mathew, Naibu Waziri, Wizara ya Maji kama ifuatavyo…

Mwisho.

Leave a Reply