You are currently viewing MFANYA BIASHARA MAARUFU MOSHI AKABIDHI MSAADA KWA WAATHIRIKA

MFANYA BIASHARA MAARUFU MOSHI AKABIDHI MSAADA KWA WAATHIRIKA

Mfanyabiashara na mdau wa maendeleo Moshi Mjini Alhaj Ibrahimu Shayo maarufu Ibra line @ibraline_filling_station amekabidhi misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika Wilaya ya Moshi Vijijini na Moshi Manispaa huku akiwarai wadau wengine kujitokeza.

Akikabidhi misaada hiyo leo kwa Mkuu wa wilaya ya Moshi katika kambi ya shule ya sekondari Lucy Larmeck iliyowahifadhi waathirika wa mafuriko hayo ameeleza kuwa lengo lake ni kupunguza ukali wa maisha na mazingira waliyopo waathirika hao kwa sasa hivyo ni vema wadau wengine kujitokeza na kuonesha uzalendo wao.

“Mimi ni mzaliwa wa Kata ya Mji mpya na familia ya Wazazi wangu pia iliathirika na mafuriko,kiasi hiki cha msaada ni mwanzo wa kuchangia wenzetu wenye changamoto,lazima tujitahidi na kuwa na roho ya kutoa, naomba wafanyabiashara na wadau wengine wajitoe ili kusaidia maisha ya wenzetu” alisema Shayo

Akipokea misaada hiyo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Zephania Sumaye amemshukuru Mfanyabishara huyo na kueleza kuwa bado mahitaji ni makubwa.

“Madhara bado ni makubwa watu 4,000 wameathirika na mafuriko,uhitaji ni mkubwa ila muamko wa watu kusaidia hauridhishi, Serikali bado inafanya jitihada ya kutoa msaada na inatoa rai wananchi walio mabondeni na ndani ya mita sitini kutoka chanzo cha mto waondoke”alisisitiza Sumaye.

Awali akiongea katika tukio hilo Diwani wa Kata ya Mji Mpya Abuu Shayo ameiomba serikali kuona umuhimu wa kuwapatia maeneo wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko kwani wamiliki wake wengi ni wazee wasiyoweza kufanya ujenzi tena,aidha amemuomba Mfadhili huyo kusaidi upatikanaji wa sare za shule kwani wanafunzi ombi ambalo lilitekelezwa na Mfanyabiashara huyo kutoa 700,000 .

Akizunguza kwa niaba ya waathirika wa mafuriko hayo Joyce Swai amemshukuru mfanyabiashara huyo kwa kuwakimbilia na kutoa sare za shule kwa wananfunzi huku akiiomba serikali iweze kuwaondoa katika kambi hiyo na kutafutiwa maeneo mengine ya kuweka makazi yao.

Miongoni mwa msaada uliotolewa ni pamoja na mahindi, mchele, ndizi, magodoro,taulo za kike, sabuni, madaftari pamoja na fedha taslimu 700,000 kwaajili ya sare za shule.

Leave a Reply