You are currently viewing MHE. SHALLY RAYMOND AHAMASISHA WANAWAKE USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

MHE. SHALLY RAYMOND AHAMASISHA WANAWAKE USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Kufuatia Tangazo la serikali la kuanza kutoa mikopo ya asilimia 10 inayotengwa na halmashauri kote nchini lililotolewa Mwezi Julai mwaka huu,

Mbunge wa Viti maalum kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Shally Raymond amewataka wanawake Mkoani humo kuhakikisha wamejisajili katika vikundi mbalimbali vya wanawake ili kuweza kunufaika na Mikopo hiyo.

Aidha Mhe. Shally amewezesha Vikundi Saba (7) vya kijiji cha Uri Tarafa ya Kibosho Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kugharamia pesa kwa ajili ya usajili wa Vikundi hivyo.

Aidha Mhe. Shally amewaeleza wanawake hao umuhimu wa kuboresha Daftari la Mpiga kura ili muda ukifika wawe na Sifa za kuchagua kiongozi wanae mtaka.

Hayo yamejili leo alipokuwa katika ziara ya kuhamasisha ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Kata ya Kibosho Kijiji cha Uri.

Leave a Reply