Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline Filling Station Alhaji Ibrahim Shayo Mapema leo amechangia kiasi cha Tsh. Milioni 7 kwa ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya St. Joseph kwenye harambee iliyofanyika hospitalini hapo.
Itakumbukwa Alhaji Ibrahim Shayo ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Hospitali hiyo na kamati ya Mipango na Fedha ambapo amewaomba wadau mbalimbali kusaidia kuchangia ujenzi huo kwani hospital hiyo inafaida kubwa kwa Manispaa ya Moshi na Mkoa wa kilimanjaro kwa ujumla.
” nawaomba Wadau tujitolee kwajili ya maendeleo ya Moshi haswa katika kuboresha huduma za Mama na Mtoto”
Pia amewakumbusha waumini wa dini ya Kikristo kusoma Matendo 20:35:
” Kunafuraha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.”
Maanayake ni kuwa, ukarimu unaotoka moyoni huleta Furaha.
Aidha Alhaji Ibrahim Shayo amempongeza Mgeni Rasmi Bw. Wille Lucas Mkurugenzi wa Hylife kwa kuendesha harambee kwa utulivu na kufanikisha kuchangisha zaidi ya Tsh. 191,000,000.
Alhaji Ibrahimu Shayo alimpongeza Muhasham Baba Askofu Minde kwa kuendesha ibada yenye maudhui ya kutoa na kufanya watu wahamasike kutoa kutokana na Maneno yaliyoingia kwenye nyoyo zao.
Alhaji Ibrahim Shayo amekuwa na muendelezo wa kuchangia katika makundi mbalimbali yanayohitaji bila ubaguzi wa aina yeyote.