You are currently viewing MORRIS MAKOI AWAPA TABASAMU LA NDIZI WAHANGA WA MAFURIKO ARUSHA CHINI, MABOGINI NA KAHE

MORRIS MAKOI AWAPA TABASAMU LA NDIZI WAHANGA WA MAFURIKO ARUSHA CHINI, MABOGINI NA KAHE

Mwenyekiti wa halmashauri ya Moshi Mhe. Morris Makoi Mapema leo ametimiza ahadi yake ambapo mnamo tarehe 10 mwezi huu aliaahidi wakazi wa Kijiji cha Mikocheni kata ya Arusha Chini kuwa atawapelekea roli 2 za ndizi kwa kata ya hiyo na Kata jirani ya Mabogini.

Aidha Mwenyekiti kwa kushirikiana na baadhi Waheshimiwa madiwani kutoka Jimbo la Moshi Vijijini na Vunjo wametoa zaidi ya Mikungu 700 ya ndizi kwa waathirika hao wa Mafuriko Mikocheni na Chemchem kata ya Arusha Chini, Kitongoji cha Bogini na Newland kata ya Mabogini na katika kambi ya Wathirika iliyopo Gona kata ya Kahe Mashariki.

Aidha pamoja na Hayo Mwenyekiti pia alipeleka mabranketi, Mafuta ya Kupikia, Pedi za Wanawake, Maji ya Kunywa, Mchele, na Mikeka akiwaasa Wathirika hao kutumia Mahitaji hayo kwa uangalifu nakwamba Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya iko bega kwa bega na wao kuhakikisha hawapati Changamoto yeyote katika kipindi hiki cha Mpito.

Pia Wananchi wa kata ya Arusha Chini walimshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri na Kuwashukuru waheshimiwa Madiwani waliokusanya ndizi hizo katika vijiji mbalimbali katika kata zao na kuwajali na kutimiza ahadi yake aliyowahidi alipokwenda kuwakabidhi Msaada wake wa Unga wa mahindi na vyandarua.

Aidha katika kitongoji cha Bogini kata ya Mabogini Wananchi walionekana kufurahia zaidi TABASAMU LA NDIZI kutokana na Mgao huo ulihusisha hata ambao hawakuathirika kutokana na uingi wa ndizi hizo huku wakiwa wamebeba Mikungu mikubwa na wakiimba nyimbo za Kuisifu Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan Raiswa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania. Katika Migao hiyo ilisimamiwa kwa karibu na Viongozi wa kamati za Maafa za kata husika.

Mhe. Makoi aliwafikishia Salamu za Mhe. Zephania Sumaye Mkuu wa wilaya ya Moshi za Kuwatakia Afya njema.

Mwenyekiti aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Fedha na uongozi Halmashauri ya Wilaya ya Moshi akiwemo, Mhe. Leonard Waziri Diwani kata ya Arusha Chini, Mhe. Dickison Tarimo – Makuyuni, Mhe. Samweli Materu – Uru Mashariki, Mhe. Prosper Masawe – Kibosho Magharibi, Mhe. Ana Peter Lyimo- Kilema Kaskazini pamoja na Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

Leave a Reply