You are currently viewing RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI KITAIFA MKOANI KATAVI.

RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI KITAIFA MKOANI KATAVI.

Na.Elisa Shunda, Dar Es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa Julai 13 mwaka huu Mkoani Katavi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, leo tarehe 29/06/2024. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM, Ndg. Ally Salum Hapi (MNEC) amesema maadhimisho hayo yataanza Julai 8 na kufikia kilele chake Julai 13 mwaka huu.

Hapi amesema Katika maadhimisho ya wiki ya Wazazi yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii na kichama,

Amesema shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo ni pamoja na ufunguzi wa Wiki ya Wazazi Kitaifa ambayo itafanyika Julai 8 Wilayani Mlele Mkoani Katavi.

Aidha amesema katika ufunguzi huo wanatarajia kupanda miti zaidi ya laki moja (100,000)

Hata hivyo amesema Rais Dkt. Samia Atawakagulia shughuli mbalimbali za ustawi wa Jamii ambazo zinafanywa na Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi na Shughuli zingine za Chama Cha Mapinduzi za usajili wa kielekroniki.

Wanatarajia pia kuwa na Kongamano la Maadili na Malezi, huku akisema Kama wanavyofahamu wanalo tatizo la mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii na tatizo hilo linafungamana na malezi.

Amebainisha kuwa Katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa kutakuwa pia na usiku wa utamaduni ambao utashindanisha vyakula vya asili vya kitanzania.

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, amesema Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha inashiriki kuhamasisha watanzania kujitokeza kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na wapiga kura wapya wajitokeze kujiandikisha.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Wazazi Kitaifa kuhamasisha Jumuiya ya Wazazi inaendelea kutoa mchango na kuhamasisha kufanyika kwa uchaguzi na watanzania kuhamasika kushiriki katika uchaguzi huo.

Mwishoo.

Leave a Reply