You are currently viewing RAIS MWINYI AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA ANGLIKANA DUNIANI.

RAIS MWINYI AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA ANGLIKANA DUNIANI.

DKT. MWINYI AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA ANGLIKANA DUNIANI WELBY.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kianglikana na Taasisi nyingine za dini kwa kudumisha amani na utulivu

Dkt. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana Duniani , Askofu Mkuu Justin Welby na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 11 Mei 2024.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Askofu Justin Welby kwa ujio wake Zanzibar.

Naye Askofu Justin Welby amempa pole Rais Mwinyi kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi

Vilevile ujumbe huo umempongeza kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Rais Mwinyi atashiriki kesho Ibada ya Maridhiano kutokana na madhila waliyofanyiwa Waafrika wakati wa Biashara ya utumwa katika Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini itakayoongozwa na Askofu Mkuu, Mhashamu Justin Welby.

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

Leave a Reply