Wakabidhi Mahindi, Mchele, Maharage, Cement na Nguo, watembelea Kituo cha Watoto yatima Kata ya Mabogini.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini Bi. RUWAICHI JACOB KAALE ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya wametembelea wahanga na familia za wananchi walioadhirika na janga la Mafuriko katika Kata za Kimochi,Mbokomu,Arusha Chini na Mabogini.
Akizungumza na wahanga hao aliwaeleza “ndugu zangu leo tumekuja leo tena kama UWT Wilaya ya Moshi Vijijini kuwapa pole kwa adhari mlizozipata kutoka na mafuriko ambazo hata zimepelekea kupoteza wapendwa wenu tunawapa pole sana,katika kuendelea kuwafariji pia tumewaletea gunia za mahindi,Cement,gunia za maharage,gunia za mchele na nguo hizi ambazo zitawasaidia na ninawahaidi kuwa tutaendelea kuwa nanyi bega kwa bega na serikali yenu niwahakikishie iko nanyi bega kwa bega pia”.
Ruwaichi Kaale
Aidha aliongeza kwa kusema “Tumefanya kwa upekee kwa Kata ya Kimochi tumesema tuwaletee chakula lakini kwa kuwa tayari zoezi la kuwajengea makazi mapya limeanza ndio maana tukawaletea pia na mifuko hii Cement ili isaidie kufanikisha Ujenzi huo”
Ruwaichi Kaale
Akizungumza wanafamilia ya Peter Kimambo, kata ya Mbokomu aliishukuru sana Umoja wa Wanawake CCM Kwa kufika leo na kuwapa pole na kusema kuwa wamefarijika sana huku wakitoa shukrani zao za dhati kwa Serikali ya Dkt. Samia Suluh Hassan kwa kuwa naobkaribu tangu wamepatwa na athari hizi na kuwaomba viongozi hao wafikishe salamu zao za shukrani pia kwa Mhe. Nurdin Babu , Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mhe.Zephania Sumaye, Mkuu wa Wilaya ya Moshi kwa msaada wao na jinsi walivyowasaidia kwa hali na mali tangu walipopatwa na janga hili na mpaka leo.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliongozana na Wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya Wilaya Ndg.Shakira Sukuru , Ndg. Mary Mkonyi , Ndg. Advela Ntangeki ,Ndg. Asia Kimaryo, Ndg. Asha Yusuph na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya Ndg. Esther Kwai.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti na Kamati yake pia waliweza kutembea kituo cha watoto yatima kilichoko katika Kitongoji cha Bogini Juu kata ya Mabogini,Kituo ambacho kiko katika maeneo ambayo pia yaliadhirika na mafuriko hayo na kuwapa neno la faraja na pole.