You are currently viewing Wanawake tumuungeni mkono Rais Samia

Wanawake tumuungeni mkono Rais Samia

Wanawake tumuungeni mkono Rais Samia

NA KIJA ELIAS, MWANGA.

WANAWAKE wametakiwa kujitoa kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,  kwa jitihada zake ambazo anazifanya katika kuwakomboa kiuchumi.

Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Afya, Malezi na Mazingira ya Baraza Kuu la Umoja wa WAZAZI (CCM) Taifa, Dk. Catherine Ndamalya, ameyasema hayo wakati  akikabidhi matofari 1,000 ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Amesema serikali imeirejesha mikopo ya asilimia 10 iliyokuwa imesitishwa kutolewa na halmashauri, ambapo kwa sasa serikali imekuja na mfumo mpya wa utoaji wa mikopo hiyo na kuwataka wanawake hao kuchangamkia fursa hiyo kwa lengo kujikomboa kiuchumi, huku akisistiza kuirejesha mikopo hiyo kwa wakati.

“Serikali imeamua mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu iliyokuwa imesitishwa hapo awali imerejeshwa kwa majaribio kuanzia mwezi Julai 2024 katika Halmashauri 10 hapa Nchini kwa mfumo mpya wa usimamizi twendeni tukachukue mikopo hiyo.”

Aprili 16, 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa  aliwasilisha hotuba kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Akizungumzia ujenzi wa nyumba hiyo Dk. Ndamalya amesema ili mtumishi aweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, anatakiwa anapotoka nyumbani kwake mazingira ya nyumba yake pia yawe salama, kupitia ujenzi wa nyumba hiyo anaimani katibu atakwenda kufanya majukumu yake ya kazi kwa ari kubwa.

“Nimekuja kujumuika na Jumuiya ya WAZAZI mkoa wa Kilimanjaro wilayani Mwanga ili kuweza kuchangia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Jumuiya yetu,”

Amesema katika taifa lolote watu ndio rasilimali kubwa na ndani ya CCM, Wana-CCM ni nguzo kubwa ya kufikia malengo ya chama, makatibu hawa tulionao, ndiyo watendaji wakuu ambao wanaratibu shughuli zote kama hawatakuwa na sehemu nzuri ya malazi hawawezi kutanya kazi za chama kwa ufanisi maana watakuwa wakifikiria kodi ya nyumba.

“Kwa utaratibu huu ulioanzishwa na Jumuiya ya umoja wa WAZAZI  Kilimanjaro wa kuwajengea nyumba za makazi watumishi wao umenigusa na mimi kuweza kuwachangia matofari 1,000 ambayo nina imani yatakwenda kukamisha boma kwa hatua kubwa.”amesema .

Dk. Ndamalya

MWISHO.

Leave a Reply