You are currently viewing Umoja wa Vijana Jipangeni vizuri katika maeneo yenu kwa ajili ya Uchaguzi

Umoja wa Vijana Jipangeni vizuri katika maeneo yenu kwa ajili ya Uchaguzi

Na Mwandishi wetu.

Moshi.Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimeutaka umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoani humo, kujipanga vizuri katika maeneo yao ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Mercy Mollel wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Moshi vijijini, mkoani humo, ambapo amesema, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi bora ambao utawawezesha kushinda uchaguzi mkuu mwakani.

“Mwenyekiti mwaka huu ni uchaguzi wa serikali za mitaa, tunahitaji kushinda uchaguzi huo ulioko mbele yetu, kwenye vijiji vyote, vitongoji vyote, mitaa na wajumbe wote watokane na chama chetu CCM”amesema Mollel

Amesema “Tunataka tushinde kwa sababu uchaguzi wa mwaka huu, ni kujenga msingi wa  nyumba yetu ya 2025 ambapo tutachagua madiwani, wabunge na Rais, hivyo tukijenga msingi imara mwaka huu, ni hakika uchaguzi wa mwakani utakuwa mrahisi kwetu”.

Aidha amesema kuomba kura katika kipulindi hiki haitakuwa kazi ngumu kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikaki kupitia Rais Samia Suluhu Hassan, na kwamba kinachohitajika ni viongozi wa vijana kufanya ziara kuelezea kazi hizo.

“Kuomba kura kipindi hiki ni rahisi, kwani ukienda Hospitalini utakuta kazi ambazo mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) amefanya, ukienda kwenye Afya, miundombinu, elimu, umeme, maji na maeneo mengine utakuta amefanya,”.

“Na kama vijana wenu hawajui, tambueni mna kazi ya kufanya ziara kwenda kuwaelezea kazi iliyofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi kupitia fedha nyingi zilizoletwa, vijana wasomi nendeni mkachambue hayo kwa wananchi kule chini kuonyesha kazi ambazo zimefanywa na serikali”

“Maandiko yanasema nimewaandikia ninyi vijana kwa sababu mnanguvu nanyi mmemshinda yule mwovu. Na niwaambie  kipindi hiki hamtakiwi kutumia nguvu kubwa kumshinda yule mwovu, ni ninyi kufanya ziara kwenye matawi yenu, mshuke hadi kwenye mashina kwenda kuelezea kazi ambazo amezifanya Rais Samia kwa kipindi cha miaka mitatu toka Mungu amkabidhi Taifa letu”.

Amesema ni juiumu la vijana pia kupita kuangalia watu wanaokubalika katika jamii, ambao wakisimamishwa kugombea, wataweza kukivusha chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

“Vjana ni Jicho, sikio na ni Pua, ninyi ndio mnaonusa ni nani anakubalika na watu wote, asimamishwe nani kwenye kitongoji, nani asimamishwe kwenye kijiji, mjumbe nani asimamishwe, hilo ni jukumu la Vijana, lakini ninyi msiwe watazamaji, msiwe wasindiizaji nanyi mjitokeze kugombea na mjiangalie wenyewe ni nani anafaa kuwa kiongozi kwa sababu si kila kijana anafaa kuwa kiongozi”.

Ameongeza “Kila mtu unapotembea muombee Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) na msimuombee kitu kidogo omba Mungu  ampe afya na  umri mrefu zaidi ili mwakani tumchague na ashinde kwa kishindo aendelee kutuletea maendeleo”

Akizungumza Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhan Mahanyu ameupongeza umoja wa Vijana katika Wilaya hiyo kwa kuendelea kuwalea vijana vyema na kuwataka kujipanga vizuri na uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Tujipange vizuri na uchaguzi wa serikali za mitaa na tuhakikishe tunashinda vijiji vyote na vitongoji vyote,”amesema Mahanyu.

Mwisho.

emmanuel

Komkya Nexus---- Komkya Nexus is a dynamic platform dedicated to delivering the latest in media updates, insightful blogs, and comprehensive business solutions. Our mission is to keep you informed and help your business thrive with expert content and innovative services. Join us and stay ahead in the ever-evolving world of media and business.

Leave a Reply