You are currently viewing ZAIDI YA WATU 4,000 WANAHITAJI MSAADA

ZAIDI YA WATU 4,000 WANAHITAJI MSAADA

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Zephania Sumaye ameeleza kuwa bado msaada zaidi unahitajika kuwafikia waathirika wa mafuriko Wilayani Moshi ili kuondoa changamoto zinazowakabili waathirika wa mafuriko.

Ametoa kauli hiyo leo Aprili 29.2024 wakati akipokea msaada wa vyakula na magodogo kutoka kwa Mfanyabiashara na mdau wa Maendeleo Moshi Mjini Alhaj Ibrahimu Shayo katika Kambi iliyo wahifadhi waathirika hao Shule ya Sekondari Lucy Lameck.

“Madhara bado ni makubwa watu zaidi ya 4,000 na Kaya zaidi ya 1000 wameathirika na mafuriko,uhitaji ni mkubwa ila muamko wa watu kusaidia hauridhishi, naomba Wakazi wa Moshi na Kilimanjaro wanayoishi Dar es salaam na maeneo mengine kuongeza nguvu ya misaada nyumbani,Serikali bado inafanya jitihada ya kutoa msaada na inatoa rai wananchi walio mabondeni na ndani ya mita sitini kutoka chanzo cha mto waondoke.” Alisema Sumaye.

Mfanyabiashara huyo ametoa misaada mbalimbali ikiwemo Magodoro,mahindi,Mchele,sabuni,taulo za kike,kalamu,madaftari na kiasi cha shilingi laki Saba kwaajili ya Wanafunzi kushonewa sare za shule.

Leave a Reply