You are currently viewing Kamati ya Bunge yataka hatua walioiangusha KCBL

Kamati ya Bunge yataka hatua walioiangusha KCBL

Kamati ya Bunge yataka hatua walioiangusha KCBL

NA KIJA ELIAS, MOSHI.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imeitaka Serikali kuwapelekea taarifa kwa maandishi ni hatua gani zilizochukuliwa kwa wale waliosababisha angako la benki ya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KCBL).

Hayo yamejiri leo Aprili 21, 2024 kwenye kikao cha Viongozi wa Vyama vya Ushirika nchi kilichoketi mjini Moshi mkoani humo, baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya siku moja, ndani ya mkoa wa Kilimanjaro, kutembelea benki ya KCBL na kupata taarifa rasimi juu ya hatua zilizofikiwa katika uanzishwaji wa benki ya Taifa ya Ushirika.

Amesema historia inaonesha kulikuwa kuna ukwasi, kipindi cha mpaka kufikia mwaka 2020 ambapo benki hiyo ilikufa kabisa ili hali kulikuwa kuna uongozi.

“Wapo watu walisababisha kukwama huko, hivyo tunapokwenda kuifufua na kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika ni lazima tuangalie ni wapi tulipoangukia, ni nani waliotusababisha tuanguke, je bado wapo miongoni mwetu  na hatua gani zimechukuliwa ili dhana ya uwajibikaji ichukue nafasi yake na  iwe funzo na mwelekeo mzuri wa huko mbele kwa wale ambao wameaminiwa katika kuianzisha na kuiendeleza benki yetu”amesema Mzuzuri.

Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Profesa Patrick Ndakidemi, amesema watu waliosababisha benki ya KCBL wamerudisha nyuma jitihada za wakulima ambao walikuwa wamewekeza fedha zao katika benki hiyo.

“Hawa watu waliosababisha hasara za fedha ambazo zilikuwa zinamilikiwa na benki ya KCBL, ukweli wamewarudisha nyuma sana wakukima wetu, lakini pia wameleta aibu kubwa kwa taifa letu,”amesema Mbunge Ndakidemi.

Profesa Ndakidemi amesema wakulima wengi, waliwekeza fedha zao katika benki hiyo, ambapo watu wachache wenye roho ya ulafi walichukua pesa za wakulima hao na kuzitafuna kitu  ambacho kimeupa mkoa wetu picha mbaya kwa jamii.

“Ninamshukuru sana Mwenyekiti wa Kamati hii ameitaka Serikali  kuipelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania taarifa kwa maandishi ili kujua hatua zilizochukuliwa kwa wale waliosababisha angako la Benki yetu ya Ushirika mkoa wa Kilimanjaro (KCBL).”

Mbunge huyo ameongeza kuwa wako baadhi ya watu wamekula pesa za watu masikini na kuzitumia huku akitolea mfano wa SACCOS ya Kindi iliyoko Wilaya ya Moshi, jambo ambalo limewasababishia wananchi hao kurudi nyuma kiuchumi kutokana na fedha hizo ambazo walikuwa wamewekeza kuwa ndio tegemeo lao.

MWISHO.

Leave a Reply