NA WILLIUM PAUL, ROMBO.
MKUU wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Raymond Mwangwala ameagiza kufanyika Oparesheni maalum katika wilaya hiyo ili kuwatambua Waganga wote wa kienyeji waliopo wilayani humo pamoja na kujua shughuli wanazozifanya.
Mwangwala alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji cha Mrere kata ta Katangara Mrere ambapo alisema kuwa serikali ya wilaya ni wajibu ipate taarifa za waganga wote wa kienyeji wanaofanya shughuli katika wilaya hiyo.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya pia aliagiza kufanyika kwa sense ya watu wote wenye ulemavu wa ngozi katika wilaya hiyo ili kutambua wapo wapo na kila mwananchi awajibike kuwalinda watu hao wenye ulemavu wa ngozi.
“Lipo tukio limetokea na mtoto Albino kuchukuliwa na kwenda kukatwa viungo wakiamini kwamba viungo vya albino vinaweza vikamtajirisha mtu hawa ni Binadamu kama sisi ni ndugu zetu hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi hata wewe lala masaa 24 uone kama chakula kitakufuata nyumbani”
alisema Mangwala.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia nafasi hiyo kuwataka Wananchi wa Rombo wanaposikia yupo mtu anachangamoto na ananusa katika kumfachia kitu chochote mtu mwenye ulemavu wa ngozi watoe taarifa mara moja.
Alisema kuwa, Wilaya ya Rombo inapinga tabia ya namna hiyo na kuahidi kuwalinda Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa gharama yoyote ili kuhakikisha wanakuwa salama.
“Sasa unayejiamini kuwa wewe ni kidume jaribu kulamba sumu kwani sumu haijaribiwi kwa kuonjwa kila mtu anayo haki ya kuishi na serikali itawalinda kwa gharama yoyote hakuna kinachokuja kirahisi rahisi wananchi tufanye kazi”
alisema Mangwala.
Mwisho….