You are currently viewing Lema: Nimesikitishwa na Uamuzi wa Msigwa

Lema: Nimesikitishwa na Uamuzi wa Msigwa

MJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa aliyekuwa kada mwenzake wa cha hicho, Mchungaji Peter Msigwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Lema ambaye pia alikuwa Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa Chadema kanda ya kaskazini, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, amesema amesikitika kwa sababu alidhani wangeendelea kuwa timu moja na kufanya kazi ya siasa kwa masilahi ya umma.
“Hata hivyo, namtakia kila la heri huko alikoenda maana kila mtu ana ndoto katika maisha yake na angependa zitimie,” amesema Lema.

Msigwa ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa ,leo tarehe 30 Juni amejiunga CCM na kupokewa na Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hiko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msigwa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza uhalali wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania.

Pia baada ya kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na Chadema.

Leave a Reply