You are currently viewing MAAGIZO YA DR. NCHIMBI KUHUSU BOOM TUTATEKELEZA KWA HARAKA

MAAGIZO YA DR. NCHIMBI KUHUSU BOOM TUTATEKELEZA KWA HARAKA

MAAGIZO YA DR. NCHIMBI KUHUSU BOOM TUTATEKELEZA KWA HARAKA

Amesema Wizara yake imepokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi dkt Emanuell Nchimbi kuhusu suala la boom kwa wanafunzi wa vyuo nchini.

Dr Nchimbi akiwa eneo la Usa River Wilaya ya Arumeru alitoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanafunzi wa vyuo wanalipwa fedha hizo ifikapo mwisho wa mwezi June.

Profesa Mkenda ambaye ni mbunge wa Rombo akizungumza kwenye kikao cha ndani cha viongozi na mabalozi wa chama cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, alisema kuwa Wizara yake imepokea agizo hilo na kwamba watalitekeleza kabla ya mwisho wa mwezi.

“Ndugu Katibu Mkuu jana pale Arusha ulitoa maelekezo kuhusu suala la boom na naomba nitumie nafasi hii kusema kuwa suala hilo tutalifanyia kazi na kabla ya muda uliyotoa wanafunzi wote nchini watalipwa” alisema.

Prof. Mkenda

Leave a Reply