Takriban watu 19 wamefariki dunia katika mji wa Tana Tojara uliopo jimbo la Celebes Kusini katikati mwa Nchi ya Indonesia, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Jumapili Aprili 14, 2024 na kusababisha maporomoko ya udongo.
Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga katika eneo hilo, Sulaiman Malia akiongea na Vyombo vya Habari amesema, Mvua kubwa iliyonyesha ilileta uharibifu katika maeneo ya makazi ya watu kando ya milima na kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyozika makazi ya eneo hilo.
Kuna vifo 19, huko Makale Kusini na vingine 15 katika vijiji vinavyozunguka Makale, kwa sasa,l bado tunatafuta waathiriwa wengine kwani watu wawili bado hawajapatikana, labda walizikwa kwenye maporomoko ya udongo,” alisema Malia.
Indonesia imekuwa ikikumbwa na maporomoko mengi ya ardhi wakati wa msimu wa mvua kutokana na ukataji miti ambapo mapema mwezi Machi, mafuriko na maporomoko ya ardhi katika kisiwa cha Sumatra yalisababisha vifo vya watu 30.