You are currently viewing MIAKA TAKRIBANI MINNE (4) YA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA JIMBO LA VUNJO

MIAKA TAKRIBANI MINNE (4) YA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA JIMBO LA VUNJO

Kwa miaka 25 (1995 – 2025) ya uwepo wa Jimbo la Vunjo likiwa limeongozwa na wabunge wanne kwa nyakati tofauti lilifanikiwa kuwa na zahanati 13 zinazotoa huduma. Katika zahanati hizo 8 zilijengwa kati ya mwaka 1958 – 1990 na 5 zingine zikiwa zimejengwa kati ya mwaka 1995 – 2015.

Miaka 4 tu katika uwakilishi wa CCM katika nafasi za uenyekiti wa serikali za vitongoji na vijiji, madiwani na Ubunge kupitia Mhe Dkt Charles Stephen Kimei chini ya serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Mhe Dkt Samia Suluhu HassanJimbo la Vunjo tumepata fedha takribani shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kujenga zahanati 12 ikiwemo Kileuo (Kata ya Kirua Vunjo Mashariki), Mabungo (kata ya Kirua Vunjo Kusini), Legho Mulo (kata ya Kilema Kusini), Njiapanda (kata ya Njiapanda), Kochakindo (Kata ya Kahe Mashariki) nk zahanati zote hizi zimekamilika na zinatoa huduma kwa wananchi. Faida wanayoipata wananchi ni kupata huduma za afya katika umbali mfupi na kwa gharama nafuu.

Upande wa vituo vya afya kwa Miaka 25 iliyopita Jimbo la Vunjo limekuwa na vituo vya afya 2 na kituo cha huduma za wagonjwa wa Nje kimoja ambavyo ni:-

  1. Kirua Vunjo – kilichojengwa 1954
  2. Mwika Msae kilichojengwa mwaka 1958
  3. Kituo cha wagonjwa wa nje (OPD) Himo kilichojengwa mwaka 2006

Miaka 4 ya Awamu ya sita na uwakilishi wa Ubunge wa Mhe Dkt Charles Stephen Kimei tumepata:-

  1. Kituo kipya cha afya Marangu Hedikota (kata ya Marangu Mashariki kilichogharimu shilingi milioni 500
  2. Kituo kipya cha Afya Kahe (Kata ya Kahe/Kahe Magharibi) kilichogharimu shilingi milioni 500
  3. Upanuzi wa kituo cha afya Kirua Vunjo kwa shilingi milioni 500
  4. Kituo cha afya Koresa (kuanza ujenzi wakati wowote)
  5. Kufanikisha kupandishwa hadhi kwa Himo OPD kuwa kituo cha afya kamili pamoja na kuongezewa wataalam wa kada ya afya, vifaa tiba, dawa na vitendea kazi vingine ikiwemo gari la Wagonjwa (Ambulance)

Mafanikio haya ni matokeo ya uongozi wa pamoja uliowezesha utekelezaji wa vitendo wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 ambayo CCM iliwakabidhi wawakilishi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Bila kupepesa macho haya ni maendeleo kwa vitendo na huwezi kuyaeleza bila kumpongeza Mbunge wa Jimbo hili la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei kwa kuwa mwakilishi anayeyajua mahitaji ya wananchi, kupaza sauti yapate bajeti na kuwa mfuatiliaji mzuri hakika amekua mwakilishi muaminifu mwenye maneno kidogo ila vitendo vyenye sauti kubwa.

Kipekee tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa kwetu wanavunjo haya ndio mahitaji na maendeleo ya watu. Hakika serikali ya Awamu ya Sita inauishi msemo huu, ‘Serikali ya watu kwa ajili ya watu’

Leave a Reply